Download

27-

اللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللَّهُمَّ اغْسِلْني مِنْ خَطَايَايَ، بِالثَّلْجِ وَالْماءِ وَالْبَرَدِ

“Ee Allaah! Niweke mbali mimi na makosa/dhambi zangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Ee Allaah! Nitakase na makosa/dhambi zangu kama Unavyoitakasa nguo nyeupe na uchafu. Ee Allaah! Nisafishe na makosa/dhambi zangu kwa theluji, kwa maji na kwa barafu.”[1]

28-

سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، وَتَبارَكَ اسْمُكَ، وَتَعَالَى جَدُّكَ، وَلاَ إِلَهَ غَيْرُكَ

“Kutakasika ni Kwako, Ee Allaah na himdi zote ni Zako. Limetukuka jina Lako, Utukufu Wako uko juu, na hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe.”[2]

29-

وَجَّهْتُ وَجْهِي للَّذِي فَطرَ السَّمَواتِ والأَرْضَ حَنيفاً وَما أَنا مِنَ الْمُشْرِكِينَ إِنَّ صَلاَتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي للهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ اللَّهُمَّ أَنْتَ الْمَلِكُ لاَ إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ ظَلَمْتُ نَفْسِي واعْتَرَفْتُ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي ذُنُوبِي جَمِيعاً فإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ واهْدِنِي لأَحْسَنَ الأَخْلاَقِ لاَ يَهْدِي لأَحْسَنِهَا إِلاَّ أَنْتَ واصْرِفْ عَنِّي سَيِّئَها لاَ يَصْرِفُ عَني سَيِّئَهَا إِلاَّ أَنْتَ لَبَّيْك وَسَعْدَيْكَ والْخَيْرُ كُلُّهُ في يَدَيْكَ وَالشَّرُّ لَيْسَ إِلَيْكَ أَنا بِكَ وإِلَيْكَ تَبَارَكْتَ وَتَعَالَيْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وأَتُوبُ إِلَيْكَ

“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambaye Ameumba mbingu na ardhi, hali ya kumtakasia Yeye Dini yangu na sikuwa mimi ni katika washirikina. Hakika Swalah yangu na kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa Allaah, Mola wa walimwengu, Yeye asiyekuwa na mshirika; kwa hilo nimeamrishwa na mimi ni katika Waislamu. Ee Allaah! Wewe ndiye Mfalme. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Wewe ndiye Mola Wangu na mimi ni mja Wako. Nimeidhulumu nafsi yangu. Nimekiri madhambi yangu. Nisamehe madhambi yangu yote. Hakika hakuna mwengine asamehae madhambi isipokuwa Wewe. Niongoze katika tabia njema. Hakuna aongozae katika tabia nzuri isipokuwa Wewe. Niepushe na tabia mbaya. Hakuna mwengine mwenye kuepusha na tabia mbaya isipokuwa Wewe. Naitikia mwito Wako na kufuata maamrisho Yako. Kheri zote ziko Mikononi Mwako. Shari haitoki Kwako. Nimepatikana kwa ajili Yako na ni Wako. Umetakasika na umetukuka. Nakuomba msamaha na ninarejea Kwako.”[3]

30-

اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَالَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَواتِ والأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ والشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادك فِيما كانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم

“Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Mikaaiyl na Israafiyl! Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ambaye ni Mjuzi wa mambo yenye kujificha na yalio ya wazi! [Siku moja] utahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana! Niongoze mimi katika haki katika yale waliotafautiana kwa idhini Yako – Hakika Wewe unamuongoza umtakaye katika njia ilionyoka.”[4]

31-

اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيرَاً، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيراً، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيراً، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً، وَسُبْحَانَ اللَّهِ بُكْرَةً وَأَصِيلاً) ثَلاثاً (أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ: مِنْ نَفْخِهِ، وَنَفْثِهِ، وَهَمْزِهِ

“Allaah ni Mkubwa kihakika. Allaah ni Mkubwa kihakika. ni Mkubwa kihakika. Himdi nyingi ni Zake Allaah. Himdi nyingi ni Zake Allaah. Himdi nyingi ni Zake Allaah. Ametakasika Allaah kutokana na mapungufu asubuhi na jioni” pia mara tatu. Ninajikinga kwa Allaah kutokamana na shaytwaan, kupulizia kwake, kutabana kwake na kutia kwake wasiwasi.”[5]

32-

اللّهُـمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ  نـورُ السَّمـواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِن ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَـيِّمُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِن  ، [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِن] [وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِن]   [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ ] [وَلَكَ الْحَمْدُ] [أَنْتَ الْحَـقّ وَوَعْـدُكَ الْحَـق ، وَقَوْلُـكَ الْحَـق  ، وَلِقـاؤُكَ الْحَـق،  وَالْجَـنَّةُحَـق ، وَالنّـارُ حَـق ، وَالنَّبِـيّونَ حَـق ، وَمـحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حق ، وَالسّاعَةُ حَقٌّ]  [اللّهُـمَّ لَكَ أَسْلَمت ، وَعَلَـيْكَ تَوَكَّلْـت ، وَبِكَ آمَنْـت ، وَإِلَـيْكَ أَنَبْـت ، وَبِـكَ خاصَمْت ، وَإِلَـيْكَ حاكَمْـت . فاغْفِـرْ لي مـا قَدَّمْتُ ، وَما أَخَّـرْت ، وَما أَسْـرَرْت ، وَما أَعْلَـنْت ] [أَنْتَ المُقَدِّمُ، وَأَنْتَ المُؤَخِّرُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ] [أَنْتَ ا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي] [أَنْتَ المُقَدِّمُ، وَأَنْتَ المُؤَخِّرُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ] [أَنْتَ إِلَهِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ] [وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ

“Ee Allaah! Himdi zote ni Zako[6]. Wewe ndiye nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye sababu ya kusimama kwa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye una ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye mfalme wa mbinguni na ardhini. Himdi zote ni Zako. Wewe ni Haki. Ahadi yako ni haki. Neno Lako ni haki. Kukutana na Wewe ni haki. Pepo ni haki. Moto ni haki. Mitume ni haki. Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki na Qiyaamah ni haki. Ee Allaah! Kwako nimejisalimisha. Kwako nimetegemea. Wewe nimekuamini. Kwako nimerejea. Kwa ajili Yako nimegombana. Nakuacha uhukumu. Nisamehe dhambi nilizozitanguliza na nilizozichelewesha, nilizozificha na nilizozidhihirisha na yale ambayo Wewe Unayajua zaidi kuliko mimi. Wewe ndiye mwenye kutanguliza na Wewe ndiye mwenye kuchelewesha. Wewe ndiye mwabudiwa Wangu, hapana mwabudiwa wa kwa haki isipokuwa Wewe. “Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”[7]

[1] al-Bukhaariy (01/181) nambari. (744) na Muslim (01/41) nambari. (598).

[2] Muslim kwa nambari. (399) na watunzi wane wa “as-Sunan”; Abu Daawuud kwa nambari. (775), at-Tirmidhiy kwa nambari (243), Ibn Maajah kwa nambari (806), an-Nasaa´iy kwa nambari (899). Tazama “Swahiyh at-Tirmidhiy” (01/77) na “Swahiyh Ibn Maajah” (01/135).

[3] Muslim (01/534) kwa nambari. (771).

[4] Muslim (01/534) kwa nambari. (770).

[5] Abu Daawuud (01/203) kwa nambari. (764), Ibn Maajah (01/265) kwa nambari. (807) na Ahmad (04/85) kwa nambari. (16739). Shu´ayb al-Arnaa-uutw amesema:

“Ni nzuri kupitia zengine.”

[6] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema hivi anaposimama usiku kwa ajili ya kuswali Tahajjud.

[7] al-Bukhaariy (03/03) na Muslim amepokea fupi mfano wake (01/532) kwa nambari. (769).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 01/09/2018